Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Sammāhat Sheikh Swahibu Shabani, Sheikh wa Mkoa wa Tabora kupitia Jumuiya ya Mashia Tanzania (Tanzania Ithna Ashari Community), leo amefungisha ndoa ya mmoja wa wanafunzi wake wa kike katika Kijiji cha Inala, mkoani Tabora.
Katika shughuli hiyo, Sheikh Swahibu Shabani pia ametoa wito kwa Waislamu wa eneo hilo kudumisha umoja, mshikamano na maelewano, akisisitiza kuwa hakuna haja ya Waislamu kugombana wao kwa wao.
Amewahimiza Waislamu kutanguliza undugu na ushirikiano, ili kuimarisha mahusiano mema miongoni mwao na kudumisha umoja wa jamii ya Kiislamu.

Maoni yako